EPL yataka mechi zake kuchezwa ugenini

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Michel Platini

Mpango wa Ligi ya Uingereza kuchezesha mechi kadhaa katika nchi za kigeni huenda ukapata upinzani mkali kutoka kwa shirikisho la soka barani ulaya UEFA.

Katibu mkuu Gianni Infantino amesema kuwa majadiliano kuhusu mpango huo yatalazimika kufanyika iwapo ligi ya Uingereza itataka kuendelea na mapendekezo hayo.

UEFA ilipinga mpango huo wa ligi ya Uingereza kwa mechi ya 39 mnamo mwaka 2008.''Hebu tuone msimamo wa UEFA.Lakini sidhani kwamba utabadilika,itabidi ujadiliwe'',alisema.

Akizungumza na viongozi katika mkutango wa michezo jijini London,afisa huyo mwenye umri wa miaka 44 aliongezea kuwa ''mipango kama hii na mapendekezo yake yako mezani kila mara na kwamba yanahitaji kujadiliwa kila mara'',.

''lakini hii leo tuna mashirikisho ya soka ambayo huchezesha mechi zake barani Asia na hilo ni miongoni mwa mipango ya kutaka kuzichezesha mechi za kitaifa za bara Yuropa.