Tofauti zazikwa uwanjani TZ

Image caption Askofu Mokiwa na akofu Sylvelster Gamanywa

Mechi ya mpira wa miguu ya aina yake iliyowakutanisha viongozi wa dini ya kiislam na kikiristo nchini Tanzania ilifanyika katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam Tanzania, lengo likiwa kuhamasisha Amani.

Image caption Golkipa Sheikh Muharami Pembe akiokoa shuti kali kutoka kwa Padre Richard Kamenya

Viongozi hao walichanganyika na kutengeneza timu mbili walizoziita Amani na Mshikamano ambapo hadi mwisho Amani ilishinda kwa bao moja.

Sheikh Alhaji Musa Salum, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam aliiambia BBC kuwa wazo la kufanya mchezo wa namna hii lilikuja baada ya kuona kuna viashiria vya kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini.

Image caption Padri Richard Kamenya akimtoka kwa kasi Sheikh Hamis Mtonga

“Tumetaka kuwaonyesha watu wetu kuwa kuna mambo tunaweza kushirikiana na watu wa Imani nyingine. Kama vile tunavyotibiwa na madaktari wakristo na madaktari wakiristo, tunachanganyika, sokoni hakuna soko la mkiristo wala mwislam, ndio maana viongozi tumekuja pamoja” Alifafanua Sheikh Ali Haji Musa Salum ambaye pia ni mwenyekiti wa Amani mkoa wa Dar es Salaam.

Naye Askofu wa Kanisa Anglikana Dar es salaam Dr Valentino Mokiwa, ameeleza kuwa tukio hili ni mfano mzuri na bila shaka litaigwa na wapenda amani duniani kote.