Van Gaal apuuza tathmini kumhusu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Van Gaal

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema lilikuwa ni jambo la kijinga kuwaambia watu kumweka kwenye mizani baada ya miezi mitatu tu tangu ajiunge na Manchester United kama kochja wa klabu hiyo

Tangu achukue usukani kama meneja wa Manchester United hapo Julai alipigiwa debe sana wengi wakisema kwamba mbinu zake zitaanza kuleta mafanikio baada ya miezi mitatu tu.

Kufikia sasa miezi mitatu imeisha tangu ajiunge na Manchester United lakini timu hiyo bado inashikilia nambari ya sita katika orodha ya timu bora katika ligi ya kadanda ya Uingereza, huku ikiwa imeshindwa mechi mbili.

Van Gaal,mwenye umri wa miaka 63, alisema: "Lilikuwa jambo la kijinga kusema miezi mitatu kwa sababu vyombo vya habari vinaongea tu kuhusu ahadi hiyo ya miezi mitatu.."

Manchester United imeshinda mechi tatu zenye ushindani mkali tangu Van Gaal kujiunga na klabu hiyo msimu huu.

Endapo watashinda mechi dhidi ya West Brom basi huo utakuwa ushindi wa tatu mtawalia katika ligi hiyo ya uingereza .

Hata hivyo Van Gaal amesema timu yake bado haijafanya vya kutosha.