Algeria yaongoza Afrika katika soka

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Algeria

Timu ya Algeria imepanda hadi nafasi ya 15 duniani mwezi huu.

Kikosi hicho cha Desert Fox ,ambacho mwezi juni kilichukua nafasi ya Ivory Coast kama timu ilio katika nafasi bora zaidi barani Afrika,ilipanda nafasi tano juu.

Timu ya Cape Verde pia ilijipatia nafasi nzuri baada ya kupanda hadi nafasiu ya 33 duniani huku ikiwa katika nafasi ya nne barani afrika.

Lakini ni kikosi cha togo kilichopanda zaidi na kufikia nafasi 73 huku kikiorodheshwa miongoni mwa mataiufa kumi bora barani Afrika.

1. Algeria (15) 2. Ivory Coast (25) 3. Tunisia (31) 4. Cape Verde (33) 5. Ghana (35) 6. Egypt (38) 7. Cameroon (40) 8. Senegal (41) 9. Nigeria (42) 10. Togo (52)