Balotelli akemewa kwa kubadilishana jezi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mario Balotelli

Mkufunzi wa Liverpool Brendan Rogers amemkumbusha mshambuliaji wa timu hiyo Mario Baloteli kuhusu utamaduni wa soka ya Uingereza na hususan ile ya Liverpool.

Baada ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Real madrid na Liverpool, mchezaji huyo raia wa kitaliano alibadilishana jezi yake na mchezaji wa kiungo cha kati Pepe Reina kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana katika mechi ya UEFA.

Wakati huo tayari Liverpool ilikuwa imefungwa mabao matatu kwa sufuri.''Nilijadiliana na Baloteli kuhusu utamaduni wa ligi ya Uingereza na tukamalizia hapo'',alisema Rogers.

Baloteli anafanya juhudu za kuimarisha ushambuliaji wake ambapo amefunga bao moja pekee katika mechi kumi.