Man U kushinda ligi, asema Ronaldo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Christiano Ronaldo

Mchezaji wa kilabu ya Real Madrid Christiano Ronaldo amebashiri kwamba kilabu ya Manchester United itashinda ligi kuu ya Uingereza chini ya ukufunzi wa Louis Van Gaal.

Kulingana na gazeti la Mirror nchini Uingereza,mchezaji huyo anaamini kwamba kilabu hiyo aliyoichezea miaka ya 2003 hadi 2009 imefanikiwa kupata meneja mwenye uwezo kuiweka timu hiyo katika kiwango ilichowekwa naaliyekuwa kocha wake Sir Alex Ferguson.

CR7 kama anavyojulikana na wengi amesema kuwa Ijapokuwa Kilabu ya Chelsea chini ya Ukufunzi wa Jose Mourinho itamaliza katika nafasi ya kwanza msimu huu,Kocha Van Gaal atafufua matumaini ya Manchester United.

''Van Gaal ni kocha mzuri ambaye ataifanya Manchester United kuwa bingwa tena na kama si mwaka huu basi mwaka mmoja kutoka sasa'',alisema Ronaldo.