QPR yaizabua Aston Villa 2 - 0

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption QPR na Aston Villa katika vita vikali. QPR imeifunga Aston Villa

Ligi kuu ya soka ya England iliendelea tena usiku wa kuamkia jumanne kwa mchezo mmoja tu kuchezwa.

QPR ndio walikuwa wenyeji kuwaalika Aston Villa katika dimba la Loftus Road ambapo wenyeji QPR walifanikiwa kuifurusha kama si kuisasambua Aston Villa kwa jumla ya mabao 2 kwa mshangao.

Matokeo hayo yameisaidia timu hiyo kupanda nafasi moja juu kutoka mkiani kwakuwa na point 7 kibindoni huku Burnley ikiendelea kuburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo.

Chelsea ndio vinara wa ligi hiyo ambao bado wanaendelea kuwa juu kileleni.