FIFA:Nigeria yapewa hadi ijumaa kuamua

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Amaju Pinnick

Nigeria imepewa hadi ijumaa kubadili msimamo wake kuhusu uamuzi wa mahakama iliyotupilia mbali uchaguzi wa maafisa wa shirikisho la soka nchini humo la sivyo FIFA iwapige marufuku kushiriki katika mchezo huo hadi May 2015.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa shirikisho la soka nchini humo (NFF), agizo hilo la FIFA ni sharti litimizwe kufikia mchana wa tarehe 31 October.

FIFA inataka bodi iliyochaguliwa tarehe 30 September kurejeshwa la sivyo ipoteze nafasi ya kushiriki katika kombe la bara Africa.

Iwapo Super Eagles haitaafikia masharti hayo itapigwa marufuku kutoshiriki katika dimba la taifa bora barani afrika.

Nigeria ndio bingwa mtetezi wa kombe hilo na inakabiliwa na tisho kubwa la kutotetea taji lake ifikiapo tarehe 17 january hadi tarehe 8 February.

Tayari mwaka huu ,Nigeria imepigwa marufuku mara mbili kutokana na hatua ya serikali kuingilia soka ya taifa hilo.

FIFA iliionya nchi hiyo mnamo mwezi Septemba na mara nyengine tena mnamo mwezi Octoba kwamba kisa chengine chochote kitasababisha taifa hilo kupigwa marufuku kwa mda mrefu.

Hatua hiyo ya FIFA ni inafuatia uamuzi wa mahakama kuu kuhusu matokeo ya uchaguzi katika shirikisho la soka nchini humo.