Kilabu za Ulaya kukutana kuhusu Qatar 22

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Moja ya viwanja vya dimba la dunia nchini Qatar

Kilabu kubwa barani Ulaya zitakutana wiki ijayo ili kutoa ombi kwa shirikisho la soka duniani FIFA kuandaa michuano ya dimba la dunia nchini Qatar kati ya tarehe 28 mwezi Aprili na 29 mwezi May .

Qatar ilikabidhiwa maandalizi ya michuano hiyo mwaka 2010 lakini tume inayotaka kuliandaa dimba hilo wakati wa baridi imekuwa ikiendelea na kazi yake.

Muungano wa vilabu vya Ulaya,kikiwemo kilabu cha Manchester,Liverpool,Barcelona na Bayern Munich unataka kuwasilisha ombi hilo ikiwemo kuanza mechi za ligi ya msimu wa mwaka 2021 na 2022 wiki mbili mapema na kucheza mechi za mwisho za kombe la FA baada ya fainali za dimba hilo.

Huku Dimba la dunia likitarajiwa May 29,hatua hiyo itasababisha kombe la FA nchini Uingereza kukamilika mwezi Juni.

Muungano huo unaowakilisha timu 214 za bara Ulaya ,unaamini hilo huenda likaathiri mashindano ya mataji ya nyumbani nchini Ufaransa na Uhispania iwapo ombi lao litapuuzwa.