Kivumbi cha ligi kuu nchini Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption wachezaji wa Liverpool wakisheherekea bao lao

Kitimtim cha ligi kuu ya England kitaendelea tena leo wakati ambapo mashabiki wa soka nchini humo na duniani kote watapata nafasi ya kuzishuhudia timu zao zikitafuta pointi tatu muhimu.

Newcastle Utd wataikaribisha Liverpool katika mchezo ambao utarushwa moja kwa moja kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC majira ya saa tisa unusu kwa saa za Afrika Mashariki.

Arsenal wao wataikaribisha Burnley, huku Chelsea nayo wakiialika QPR. Everton watakuwa nyumbani kucheza Swansea City. Hull City wataikabili Southampton. Michezo mingine ni itakayochezwa siku hiyo ya kesho ni kati ya Leicester City watakapo kwaana na West Brom, Huku Stoke City watakapoikabili West Ham utd.

Siku ya jumapili ni mpambano wa kukata na shoka ambapo Manchester United wataavaana na Manchester City mechi ambayo pia itatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ,huku Tottenham watakapokwaana na Aston villa.

Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako