Uefa: Leverkusen yairarua Zenit 2-1

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hulk mchezaji wa timu ya Zenit St. Peterburg ya Urusi

Mchezo wa mapema wa ligi ya mabingwa Ulaya umemalizika kwa Bayer Leverkusen ya Ujerumani kuishushia kipigo Zenit St Petersburg ya Urusi cha mabao 2-1

Zenit wakiwa nyumbani wameshindwa kutamba na kuutumia vizuri uwanja wao na kuruhusu kichapo hicho.

Mchezaji Solomon Rondon aliyeingia kipindi cha pili ndiye aliyewapatia wenyeji bao la kufutia machozi huku Heung-Min Son akiifungia Leverkusen mabao yote mawili katika kipindi cha pili.

Michezo mingine saba itakayochezwa leo ikiwemo ile ya mabingwa watetezi Real Madrid na Liverpool inasubiriwa kwa hamu muda mfupi ujao.