Kocha mashakani kwa kuwabagua wachezaji

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mchezaji wa zamani wa Ufaransa Lilian Thuram na mwenzake Willy Sagnol ambaye ndio mkufunzi wa kilabu ya Bordeaux

Kocha wa klabu moja ya kandanda nchini Ufaransa anakabiliwa na shutuma kali kufuatia matamshi yake kuwa wanasoka kutoka afrika hawana maarifa

Kwenye mahojiano na gazeti moja Willy Sagnol alisema kuwa wanasoka kutoka Afrika wana nguvu lakini mchezo wa soka unahitaji maarifa, mbinu na nidhamu.

Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Lilian Thuram ameyakashifu matamshi ya kocha huyo huku chama kinachopambana na ubaguzi wa rangi kikitaka kocha huyo kuchukuliwa hatua.