Kocha apinga soka ya Marekani ,Wembley

Haki miliki ya picha PA
Image caption Roy Hodgson

Kocha wa timu ya soka ya England Roy Hodgson amehoji uamuzi wa chama cha soka nchini humo FA kuruhusu mechi ya mchezo wa soka ya marekani kuchezwa kwenye uwanja wa Wembley siku sita tu kabla ya mapambano ya soka kuwania kufuzu katika fainali za kombe la Ulaya kati ya England na Slovenia

Mchuano wa jumapili hii kati ya Jacksonville Jaguars na Dallas Cowboys ni wa tatu kuchezwa katika huo mwaka huu.

Hodgson analalamika kuwa mchezo wa soka ya marekani unaharibu uwanja na hivyo kuna uwezekano wa kupoteza ladha halisi ya mchezo wa kabumbu…

Bodi ya FA iliweka vikwazo kwa uhusiano wa chama cha rugby na uwanja huo, hata hivyo makubaliano yao yameingia mwaka wa nane sasa na zimesalia mechi zingine tatu za mwaka wa 2015. Ikiwemo ile ya Oktoba 4 siku tano tu kabla ya mechi ya mwisho ya nyumbani ya kufuzu kati ya England na Estonia