Je,Liverpool itazuia kasi ya Chelsea?

Haki miliki ya picha PA
Image caption Diego Coast ashangilia baada ya kufunga bao

Kurudi kwa viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea uwanjani Anfiled jumamosi kunarejesha kumbukumbu zisizofurahisha kwa upande wa Liverpool pamoja na hali yao ya baadaye ambayo si nzuri sana.

Ni miezi sita tu ambapo kuteleza kwa nahodha wa Liverpool Steven Gerard kuliisaidia Chelsea kupata ushindi muhimu dhidi ya timu hiyo ya Mersyside, mechi ilioathiri matokeo ya liverpool na ari yao ya kuwania taji la ligi hiyo.

Awali mwishoni mwa mwezi Aprili ,kombe hilo lilionekana likinyemelewa na Liverpool.

Haki miliki ya picha g
Image caption Raheem Sterling

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Diego Coast ataanza dhidi ya Liverpool katika mechi ya jumamosi.

Mchezaji huyo wa Uhispania amekuwa akiugua jeraha la paja na aliorodheshwa katika kikosi dhidi ya Maribor katikati ya wili lakini hakucheza.