B Rodgers: Motisha wa Liverpool umeshuka

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers asema motisha wa LIverpool umeshuka

Mkufunzi wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa kikosi chake kinakabiliwa na wakati mgumu baada ya kupoteza mechi yake ya jumamosi dhidi ya viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea kwa 2-1.

Liverpool ndio ilioanza kufunga bao la kwanza kupitia mchezaji wake Emre lakini mabao ya Garry Cahil na Diego Coast yalizima matumaini ya Liverpool na kushindwa kwa mara ya tatu mfululizo.

''Tutaimarika ,lakini kwa sasa ni wakati mgumu'',.alisema Rodgers.

Wachezaji wangu wanajaribu kila njia lakini kila tunaposhindwa motisha unazidi kurudi chini'',Aliongezea.

''Hatujafunga mabao tunayohitaji wa kufikia kiwango tunachotaka katika mchezo wetu miaka kadhaa iliopita'',alisema Rodgers.

Timu hiyo ilimaliza ya pili nyuma ya Manchester City msimu uliopita lakini kwa sasa wameshindwa kwa alama 15 na Chlesea huku ikiwa imecheza mechi 11.