ManCity yaponea huku United ikishinda

Haki miliki ya picha
Image caption Juan Mata Kushoto na Meneja Louis Van Gaal

Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City wamewachwa kwa alama nane na viongozi wa Ligi hiyo kufikia sasa Chelsea baada ya kung'ang'ania sare ya moja kwa moja dhidi ya QPR.

Juhudu za mapema za mshambuliaji wa Rangers Charlie Austin ziliambulia patupu.

Mda mchache baadaye Austin aliifungia QPR bao la kwanza lakini mda mchache kabla ya kipindi cha mapumziko Sergio Aguero alifanya mambo kuwa moja kwa moja.

Krosi murua ya Austin ilimlazimu beki Martin Demichelis kujifunga lakini Aguero alimchenga kipa Rob Green ili kusawazisha.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mancity

Wakati huohuo Manchester United ilipanda hadi nafasi ya sita baada ya Juan Mata kuifungia timu hiyo bao la pekee katika kipindi cha pili licha ya kusumbuliwa na Crystal Palace.

Katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilishindwa kuona lango la mwengine huku Fraizer Campbel wa Palace akishindwa kufunga bao la wazi naya Luke Shaw akishindwa kucheka na wavu.

Mkufunzi wa Man Utd Louis Van Gaal alimuingiza Mata baada ya saa moja kabla ya kufunga bao hilo.