V Gaal:Itachukua miaka 3 kuijenga Man U

Haki miliki ya picha AP
Image caption Louis Van Gaal asema kikosi cha Man Utd KItaimarika baada ya miaka mitatau

Mkufunzi wa timu ya Man United Louis Van Gaal amesema kuwa huenda ikachukua miaka mitatu kwa kilabu hiyo kuafikia kiwango chake.

Baada ya kupoteza moja bila dhidi ya wapinzano wao wa jadi na kuishinda QPR siku ya jumamosi Man U ina alama 16 katika mechi kumi walizocheza ikiwa ni rekodi mbaya zaidi kuwekwa na kilabu hiyo tangu mwaka 1986.

Van Gaal amesema kuwa huenda harakati za kuimarisha kilabu hiyo zikachukua miaka mitatu na kwa sasa anawahurumia mashabiki na bodi ya manchester amba amesema kuwa wana imani kubwa naye.

Manchester United ilivunja rekodi ya kuwasajili wachezaji wakati wa dirisha la uhamisho pale walipomnunua Angel Di Maria kutoka kioabu ya Real madrid kwa pauni millioni 59.7 katika msimu wa joto ,lakini wameshinda mechi nne kufikia sasa.