Morocco yashindwa kuamua kuhusu ACN

Haki miliki ya picha CAF
Image caption Morocco imeshindwa kuamua iwapo itaanda mashinda ya dimba la bara afrika 2015.

Morocco imeshindwa kufanya uamuzi iwapo itaandaa mechi za kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika za mwaka 2015.

Morocco ilikuwa imetuma ombi la kutaka kuahirishwa kwa mechi hizo kutokana na hofu kuwa mashabiki kutoka nchi za nje ambao watahudhria mechi hizo wanaweza kusambaza ugonjwa wa Ebola, lakiki shirikisho la kandanda barani afrika CAF lilikataa ombi hilo.

Mwandishi wa michezo wa BBC anasema kuwa hakuna nchi nyingine ambayo imetangaza kuchukua nafasi hiyo .

Afrika kusini iliandaa kombe hilo mwaka uliopita na tayari imesema kuwa haitaliandaa tena.