Mechi ya kutimua HIV yachezwa UG

Image caption Rais Museveni akisakata kabumbu Uganda

Uganda imeungana na mataifa mengine duniani katika vita vya maambuzi mapya ya virusi vya ukimwi ijulikanayo “Linda goli “yaani Protect the goal.

Kampeini hiyo ilizinduliwa Jumapili na Rais Yoweri Museveni wa Uganda katika mechi ya soka ya kirafi iliyochezwa katika uwanja wa Mandela mjini Kampala.

Katika hotubu yake ya uzinduzi Rais Museveni alitaja mambo muhimu manne ya kuzingatia ambayo kwanza ni kujizuia kufanya ngono za kiholela, pili kama ukishindwa kujizuia tumia mpira wa Kodomu, tatu ni kujipima damu yako kujuwa kama una virusi vya ukimwi kama unavyo uanze kutumia madawa ya kupunguza makali, na nne Mama wajawazito kuanza kutumia madawa kama wamepatwa na virusi ili mtoto asipate maambakuzi ya virusi anapozaliwa.

Rais Museveni amesema ndiyo sababau leo tumetumia mchezo wa mpira kutowa ujumbe kuwwalenga vijana

Serikali ya Uganda kupitia wizara ya afya na Shirika la umoja wa mataifa la misaada ndiyo walioshirikiana katika kampeni hiyo ambapo mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa mataifa la kutoa misaaada katika kanda ya Afrika mashariki na kusini Sheila Tlou, alisema kampeni hii wametumia mchezo wa mpira kwani inaalenga zaidi vijana.

Vijana inasemelana ndio wlaio katika hatari kubwa ya kupata maambuzi mapya ya HIV.

Mechi ya soka ilichezwa kati ya Uganda Cranes na Ethiopia ambapo Cranes waliondoka kifua mbele kwa magoli 3 kwa 0.

Kabla ya mechi hiyo wabunge wa Uganda waliwacharaza Baraza la mawaziri wa Uganda magoli 3 kwa 0.