Wandishi wanawake huru kutizama voliboli Iran

Haki miliki ya picha isna
Image caption Wanawake wakihudhuria mashindano ya Voliboli nchini Iran

Vyombo vya habari nchini Irahn , vinaripoti kwamba wandishi habari wa kike wataruhusiwa sasa kwenda kutizama mechi za voliboli.

Hii inakuja huku kukiwa na mjadala kuhusu kufungwa jela kwa mwanamke mmoja nchini humo kwa kupinga marufuku iliyopo dhidi ya wanawake kuhudhuria mashindano ya michezo.

Mchezo wa voliboli ni maarufu sana nchini Iran.

Kwa hivyo uamuzi wa bodi inayosimamia michezo kuiondolea nchi hiyo haki ya kuandaa mashindano ya kimataifa, huenda ukabatilishwa.

Marufuku hiyo iliwekwa pale ambapo mwanamke huyo Ghonceh Ghavami alipokamatwa na kufungwa.

Alikamatwa mwezi Juni wakati wa maandamano ya kupinga marufuku dhidi ya wanawake kuhudhuria mashindano pamoja na wanaume.

Maandamano hayo yalifanyika nje ya uwanja wa michezo wa Tehran, ambako timu ya taifa ya Voliboli ilikuwa inajiandaa kucheza.

Kuna tetesi kuwa mwanamke huyo amefungwa jela mwaka mmoja ingawa taarifa hizo bado hazijathibitishwa.

Kuwaruhusu wanawake waandishi wa habari kuhudhuria mashindano ya michezo ni hatua ndogo tu ya kuondoa kero iliyotokana na mwanamke huyo kukamatwa.