Mesut Ozil , Baba yake wana mgogoro

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mchezaji wa kimataifa wa ujerumani na Arsenal, Mesut Ozil

Uhusiano kati ya mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani na Arsenal Mesut Ozil na Baba yake Mustafa Ozil huenda ukawa umesambaratika kutokana na mabishano ya kisheria.

Mustafa aliifikisha kampuni ya masoko ya mwanaye mahakamani akidai pauni 495,000 za mapato yaliyopotea kwenye mkataba wa udhamini huku Mesut naye akidai kurejeshewa mkopo wake wa pauni 800,000

kesi hiyo mwishowe ilifikia tamati nje ya mahakama mwezi uliopita, lakini Mahakama imethibitisha hatua hiyo wiki hii.

Kaka wa Mesut aitwaye Mutlu amekua akisimamia shughuli za ndugu yake kwa kipindi cha mwaka jana baada ya Mesut kumfukuza kazi baba yake.

Hadi kufikia mwaka uliopita, Mustafa Ozil alikua wakala wa mwanae, na pia Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya masoko ya Mesut huku akishiriki kusimamia uhamisho wa Mesut kutoka Real Madrid kwenda Arsenal kwa pamoja na mkataba wa mamilioni ya pauni kwa kampuni ya Adidas inayomdhamini mwanaye huyo.

Akizungumza na Gazeti la Express la mjini Cologne wiki hii, Mustafa Ozil amedai kuwa mpenzi wa mwanae Mandy Capristo ndiye aliyevuruga uhusiano wake na mwanae.