Enyeama ni chaguo lako?

Vicent Enyeama

Haki miliki ya picha
Image caption Vincent Enyeama huenda akawa Golikipa wa kwanza kutwaa tuzo ya BBC

Kutoka kufahamika kuwa Golikipa bora barani Afrika,Vincent anahesabika kuwa bora barani ulaya.

Anaichezea klabu ya Lille.Msimu uliopita alijipatia heshima kwa kuweka rekodi ya kuvutia.

Mchezaji huyu,(32) raia wa Nigeria ameweka rekodi nzuri kwa msimu wa mwaka 2013-2014, jumla alidaka mikwaju 21 msimu uliopita kuliko golikipa mwingine yeyote katika magolikipa bora watano katika ligi za Ulaya.

Mwezi Mei Enyiema alipewa jina la mchezaji bora wa Afrika wa msimu katika ligi kuu ya Ufaransa.

Pia alitangazwa kuwa golikipa wa nne bora katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil

akiwa Raia wa Nigeria wa kwanza kupata tuzo ya Marc-Vivien Foe nchini ufaransa, Enyeama pengine atakua golikipa wa kwanza kushinda tuzo za BBC