Yaya Toure kuchukua tuzo ya BBC?

Yaya Toure

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure

Ni mchezaji bora Afrika, kiungo huyu wa kati kutoka Ivory Coast alishinda tuzo hizi kwa mara ya kwanza mwaka 2013.

Wakati huo aliiambia BBC kuwa tuzo hizi ni kitu cha kipekee.

Toure(31) ushindi kwake ni muhimu kwenye soka, nimshindani anayeogofya ambaye ameonesha kuwa ni mtu wa thamani katika klabu yake na hata nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Katika michuano ya Brazil mwaka huu Toure hakuonesha kiwango cha juu cha mchezo baada ya kuondokewa na kaka yake .

Lakini ameendelea kuwa mchezaji wa kutumainiwa na Manchester City tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2010.

Kutofanikiwa kwa timu ya Ivory Coast ni moja kati ya vitu vichache vilivyomkosesha Toure kuzoa tuzo nyingi.

Na kwa mara ya sita,anawania tuzo ya BBC