Xavi:Messi atawakoroga walinzi EPL

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji Lionel Messi akiifungia timu yake ya barcelona

Mchezaji Lionel Messi atawika zaidi katika ligi ya Uingereza iwapo atapata fursa ya kucheza katika ligi hiyo.

kwa mujibu wa mchezaji mwenza wa Barcelona Xavi Hernandez,Messi amejiimarisha vilivyo katika kipindi chaz miaka kumi katika ligi ya uhispoania kwa kushinda makombe matatu ya kilabu bingwa barani ulaya,mataji manne ya mchezaji bora duniani huku akitarajiwa kuvunja rekodi ya la liga kwa kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi akiwa na umri wa miaka 27 katika ligi hiyo.

Kulingana na mtandao wa Goal Dot com Wengi nchini Uingereza wanajaribu kufikiria ni vipi mchezaji huyo atakuwa iwapo atajiunga na kilabu moja nchini Uingereza.

Lakini Xavi amesema kuwa mchezaji huyo atawakoroga walinda lango wa upinzani nchini Uingereza zaidi ya anavyowafanya nchini uhispania.

Vilevile Xavi amempongeza mkufunzi wa timu ya Manchester United Louis Van Gaal kwa kumpa fursa ya kuichezea timu ya Barcelona.