Michezo ya kufuzu fainali za Euro 2016

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nani kufuzu kushiriki michuano ya mwaka 2016?

Michezo kadhaa imepigwa kuwania kufuzu fainali za Euro mwaka 2016

katika kundi A, Uholanzi imeichapa Latvia mabao 6-0,Jamuhuri ya Czech imetoka kifua mbele kwa mabao 2 dhidi ya 1 la Iceland, Uturuki nayo ikaiadhibu Kazakhstan kwa 3-1

Katika kundi B

Ubelgiji na Wales walitoka sare ya kutofungana, Cyprus imeitandika Andorra mabao matano bila majibu na Israel imeichapa Bos Herce mabao matatu kwa sifuri.

Kundi H lilikutanisha Azerbaijan na Norway ambapo,Norway iliondoka na ushindi wa goli moja kwa sifuri, Bulgaria ikatoka sare ya moja kwa moja na Malta, halikadhalika italia ilitoka sare ya moja kwa moja na Croatia.