FIFA yawasilisha lalama kuhusu michuano

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa FIFA Sepp Blatter

FIFA imewasilisha lalama yake dhidi ya watu binafsi walioshirikishwa kuandaa michuano miwili ijayo ya kombe la dunia.

Rais wa FIFA Sepp Blatter amechukua hatua hiyo kutokana na ushauri wa jaji Hans-Joachim Eckert ambaye ripoti yake iliiondolea lawama Qatar na Urusi kuandaa madimba hayo ya mwaka 2018 na 2022.

''Hakuna ushahidi wa kutosha wa kuzuia kufanyika kwa mashindano hayo'',. Alisema Eckert.

Ijapokuwa ripoti hiyo imekosolewa na wengi ,Blatter amekataa wito wa ripoti hiyo kuwekwa wazi.

''Iwapo Fifa itachapisha ripoti hiyo basi tutakuwa tunakiuka sheria za shirikisho hili pamoja na sheria za mataifa'',. Alisema Blatter.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rais wa Urusi akifurahia kuchaguliwa kwa Urusi kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018

Hatahivyo Fifa ina wasiwasi kuhusu maswala fulani.Ilisema katika taarifa yake;''kuna mambo ambayo yanaonyesha wasiwasi','.

Blatter amesema kuwa hatua hiyo inaonyesha kwamba FIFA haipingi uwazi.aliongezea kwamba ''iwapo kuna chochote cha kuficha tusingeliwasilisha swala hili katika afisi ya mkuu wa sheria''.

Eckert aliishauri Fifa kwamba makosa ya kihalifu ni sharti yawasilishwe wakati atakapotoa ripoti hiyo.