CAF:Wachezaji wawili wafariki

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Issa Hayatou

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika Caf Issa Hayatou ametuma risala za rambirambi kwa familia za wachezaji wawili wa soka ambao walifariki mwishoni mwa juma.

Aliyekuwa mchezaji wa Cameroon Vallery Mezague alipatikana amefariki katika mji wa Ufaransa wa Toulon huku mchezaji wa Guinea Oumar Tourade wa kilabu ya As kaloum akifariki kutokana na mshtuko wa moyo nchini Tunisia.

''Nimeshtushwa na kifo cha ghafla cha mchezaji huyu mchanga ambaye alikuwa ameanza vizuri kazi yake.

CAF na soka ya Afrika imehuzunishwa sana na visa vya wachezaji kuaga dunia wakiwa katika uwanjani na wengine nje ya viwanja''alisema Hayatou.

''Lengo letu sasa litakuwa kufanya utafiti wa matibabu ili kusaidia kukabiliana na maswala kama haya ili kupunguza matukio kama haya'',aliongezea Hayatou.

Valery Mezague alikichezea kilabu cha Portsmouth katika ligi ya Uingerewza ya EPL.

Mabingwa hao wa Guinea walikuwa wakijiandaa kwa msimu mpya huko Souse na Bangoura alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya kupata mshtuko wa moyo katika uwanja wa ndege wa Tunisia.