Ebola:Wanasoka mahiri kusaidia WHO

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Christiano Ronaldo

Wachezaji nyota wa kandanda duniani, Chiristiano Ronaldo wa Real Madrid, Neymar wa Barcelona, Didier Drogba wa Chelsea na Philip Lahm wa Bayern Munich wanaunga mkono juhudi za wataalam wa kimataifa wa Afya katika kuhamasisha dunia kuhusu vita dhidi ya janga la Ebola.

Katika kampeni hii mpya inayojulikana Kama "11 against Ebola" Wachezaji katoka Klabu za ulaya, wameungana kupigia debe mbinu za kuzuia kuenea kwa janga la Ebola katika jamii zilizoathirika

Wakitumia Kauli mbiu " together we can beat Ebola" kwenye mitandao ya kijamii, waneweza kujibu maswali 11 ya Kawaida ya Afya yaliyochaguliwa na wataalam wa Afya kutoka Afrika.

Shirika la Afya duniani ni baadhi ya mashirika yanayoshugulikia janga Hilo

Kila ujumbe unaeneza kupitia filamu za kuiga, kwenye redio, bendera na picha za Wachezaji hao.

Mkurugenzi mkuu wa Benki ya dunia Jim Yong Kim alisema " inavutia kuona Wachezaji bora duniani wanaungana kupitia vita janga hili"

Benki kuu ya dunia itachangisha dola bilioni moja kusaidia nchi zilizokumbwa na janga la Ebola

Mchango huu unajumuisha dola milioni 500 za shughuli za dharura na kuwatuma wafanyakazi wa Afya kutoka nchi za kigeni kusaidia Afrika.

Kuongezea, dola milioni 450 kutoka kwa shirika la kimataifa la kifedha, Ambayo iko Chini ya Benki kuu duniani, Itawezesha uwekezaji, biashara na ajira huko Guinea, Liberia na Sierra Leone nchi zilizoathirika zaidi kutokana na Ebola..