Ivory Coast yakabiliwa na vikwazo

Image caption Mashabiki wa Ivory Coast wavamia uwanja baada ya timu yao kufuzu katika dimba la bara afrika

Timu ya soka ya Ivory Coast huenda ikakabiliwa na vikwazo baada ya mashabiki wake kuvamia uwanja mjini Abidjan baada ya kupata fursa ya kuwakilishwa katika michuano ya mataifa ya bara Afrika.

kisa hicho kilitokea baada ya timu hiyo kupata sare ya bila kwa bila dhidi ya Cameroon siku ya jumatano ili kuhakikisha kuwa wanamaliza wa pili katika kundi Da.

Shrikisho la soka barani Afrika CAF limesema kuwa linasubiri ripoti ya refa kuhusu kisa hicho.

Kisa hicho huenda kikaangaziwa na kamati ya maandalizi mnamo tarehe mosi mwezi Disemba.