Je,ni Wellbeck ama Van Persie?

Image caption Wellbeck na Wilshere kuongoza Arsenal

Huku Kilabu ya Manchester ikichuana na wapinzani wao wa jadi Arsenal,Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amechelewesha hatua yake ya kutaka kumnunua kabisa mchezaji Radamel falcao kutokana na jeraha alilopata mchezaji huyo.

Falcao amekumbwa na matatizo ya jeraha pamoja na kushuka kwa kiwango chake cha mchezo tangu ajiunge na Manchester kwa mkopo kutoka kilabu ya Monaco.

Mshambuliaji huyo hajashiriki katika mechi yoyote tangu apate jereha hilo mwezi uliopita wakati wa mazoezi.

Hii leo Manchester United itamtegemea mshambuliaji wake Van Persie,nahodha Wayne Rooney na Di Maria kutafuta ushindi ambao huenda ukaipa motisha ya kupata matokeo mazuri katika michuano iliosalia.

Wakati huo Kilabu ya Arsenal itamtegemea Mshambuliaji wake Giroud pamoja na aliyekuwa mshambuliajia wa Manchester Wellbeck kutafuta mabao katika safu ya mbele.

Giroud ambaye amekuwa na jeraha anatarajiwa kuiongoza safu ya mashambulizi huku Wellbeck akichezeshwa upande wa kushoto wa safu ya mashambulizi.

Je,Welbeck atageuka na kuwa mwiba dhidi ya kilabu yake ya zamani? Ni kitendawili ambacho ni mchezaji huyo pekee anayeweza kukitegua.