Wenger alaumu walinzi wa Arsenal

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha wa arsenal Arsene Wenger amewalaumu walinzi wa timu hiyo kufuatia ushindi wa manchester United

Mkufunzi wa Arsenal Arsene wenger amesema kuwa safu ya ulinzi ya Arsenal ni hafifu baada ya kushindwa 2-1 na Manchester United katika uwanja wa Emirates.

Arsenal walipatikana wakiwa wazi katika safu ya nyuma walipojaribu kutafuta bao la kukomboa baada ya Kieran Gibs kujifunga.

Wenger amesema kuwa kwa sasa safu hiyo ya ulinzi haina uzoefu wa kutosha kuweza kusoma mechi.

Katika mechi hiyo Arsenal walifanya mashambulizi 23 katika lango la Manchester United.

Wenger aliongezea;''ni mechi tuliotawala kwa asilimia 80 na hatujatawala mechi kama hivo kwa mda mrefu'',.

''Mwisho wa mechi hatukuwa imara katika safu ya Ulinzi na tulifanya makosa ambayo walichukua fursa na kutuadhibu'',.