Shabiki amng'ata mwenziwe Kenya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wayne Rooney

Mwanamume mmoja mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya, alimng'ata sikio jirani yake baada ya mechi ya soka ya ligi ya uingereza iliyokuwa na matokeo yasiyo ya kuridhisha kwa mmoja wao.

Mwanamume huyo ambaye ni shabiki sugu wa klabu ya soka ya Arsenal aliamua kujiondolea hasira ya klabu yake kushindwa na Manchester United kwa kumng'ata hasimu wake wa Man U sikio lake Jumamosi usiku.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa shabiki huyo sugu wa Arsenal hangeweza kustahimili kukejeliwa na jirani yake shabiki wa Man United baada ya klabu yake kushindwa mabao mawili kwa moja

Mwanamume huyo alifungiwa katika chumba kimoja na wakazi wa mtaa wa Railways mjini humo, ambao walitaka kumuua kwa kitendo chake. Inadaiwa hii ni mara ya pili kwa mwanamume huyo kumng'ata mwenziwe sikio kwa sababu za kisoka.