Henry ataka kuisaidia Arsenal

Image caption Thiery Henry

Uwezekano wa Thiery Henry kujiunga na Arsenal kama mkufunzi umeongezeka baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kufichua kwamba bado ana ndoto ya kuisadia Arsenal kushinda taji la kilabu bingwa barani Ulaya.

Henry huenda akaweka viatu vyake vya soka chini jumamosi wakati ambapo kilabu yake ya New York Red Bulls itajaribu kulipiza kichapo cha mabao 2-1 ugenini katika fainal ya raundi ya pili dhidi ya New England Revolution.

Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amekamilisha kandarasi yake na kilabu hiyo na ijapokuwa anasema kuwa hakuna kilichoafikiwa kuhusu hatma yake ameanza kutoa maoni yake kuhusu maisha yake baada ya kusakata soka.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsene Wenger

Na baada ya kocha Arsene Wenger kumfungulia milango mchezaji huyo ,Henry amesema kuwa angependelea kuisaidia kilabu yake ya zamani.

''hakuna kilicho wazi''Henry aliliambia gazeti la L'Equipe.''Sijafanya uamuzi wowote na mimi sipendelei uvumi'',.

''Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba nitasalia katika soka kama mkufunzi ama afisa mkuu ,lakini tutaona'',alisema.