Mwanasoka bora kutangazwa leo na BBC

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yaya Toure

Washiriki wanne walishiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil, ambapo kwa mara ya kwanza katika hoistoria ya michuano hiyo, Timu za Afrika ziliondolewa katika hatua ya makundi.

Golikipa Enyeama alichezea Nigeria katika hatua ya 16 bora, huku Brahimi alifika kwenye hatua hiyo hiyo alipokuwa akiichezea Algeria.

Enyeama,32, alirudi kwa ajili ya ligi ya Ufaransa, alifanikiwa kucheza michezo 21 bila goli lake kuguswa.

Haki miliki ya picha
Image caption Yacine Brahimi

Nchini Hispania, jitihada za mshambuliaji Brahimi akiichezea timu yake ya Granada zikamfanya kuteuliwa kuwa mwanasoka bora wa kiafrika nchini humo msimu uliopita na kumuwezesha kujiunga na timu ya Porto.

Wachezaji wote hawa walichezea timu zao kwa umahiri na kuvutia wapenzi wengi wa soka, kama ilivyo kwa Gervinho wa Ivory Coast.

Mchezaji huyu wa Roma, amekuwa wa kutumainiwa tangu alipoachana na ligi kuu ya Uingereza alipokuwa akiichezea Arsenal, ana rekodi ya kufunga magoli 10 katika michezo 39 katika ligi ya Serie A.

Haki miliki ya picha
Image caption Gervinho

Gervinho na mwenzake Toure hawakufanya vizuri kwenye kundi lao katika michuano ya nchini Brazil, lakini wote wameeleza kufurahishwa na michuano ya msimu huu.

Mchezaji kiungo, Toure aliiongoza Manchester City kunyakua kombe la ligi kuu kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.pia alishinda michuano ya kombe la Capital One.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aubameyang

Ingawa mshambuliaji Aubameyang hakucheza michuano ya Kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 sababu Gabon haikufuzu, amekuwa katika orodha ya wachezaji bora kwa mara ya pili kwa sababu ya kuwa na msimu mzuri kwenye Bundes Liga.

Mchezaji huyu 25,amekuwa akiichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani, na jitihada zake zimeonekana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya,ambapo tayari amechoma nyavu mara tatu katika michuano ya sasa.