Barnes:Gerrard bado mzuri kwa Liverpool

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Steven Gerrard bado ana kiwango cha juu kuendelea kuitumikia Liverpool

Winga wa zamani wa Klabu ya Liverpool John Barnes anaamini kiungo na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard, bado ni mzuri vya kutosha kuendelea kuitumikia liverpool

"Katika hatua hii ya kazi yake, bado ni bora kabisa na uzuri wa kutosha kwa ajili ya Liverpool bado," Barnes alisema.

Barnes alitumia misimu 10 katika uwanja wa Anfield kabla ya kuondoka na kujiunga na Newcastle United katika umri ambao anao Gerrard hivi sasa.

Pamoja na ufanano wa umri ambao Barnes aliihama liverpool winga huyo anaimani Gerrard ana nafasi yakuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka atakapostaafu soka.

"Bila shaka tunajua ubora wa Gerrard ulivyokua nyuma, na tunajua nini huwatokea wachezaji wengi wanapofika mwisho wa kazi zao,bado ni mchezaji muhimu sana kwa klabu ya Liverpool”.

tayari liverpool kupitia meneja wake Brendan Rodgers imetangaza kumpa ofa ya mkataba mpya. Steven Gerrard utakao muwezesha kumalizia kipaji chake kwa majogoo wa jiji la London.