Rooney kufanyiwa uchunguzi zaidi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wayne Rooney

Nahodha wa Manchester united Wayne Rooney, atafanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo la goti lake.

Rooney 29 aliukosa mchezo wa jana dhidi ya Stoke City uliomalizika kwa man united kupata ushindi wa 2 kwa 1, jeraha hili la goti alilipata katika dakika za mwisho za mchezo mwa ligi kuu ulofanyika jumamosi iliyopita kwenye mchezo na Hull City.

Meneja Louis van Gaal, amesema, "atafanyiwa uchunguzi zaidi naimani jeraha sio kubwa hivyo ila tunasubiri majibu ya uchunguzi”.

Bosi huyo wa man united anaamini Rooney na Di maria hawawezi kuwa fiti kuweza kuwakabili Southampton,

United imekua ikiandamwa na majeruhi wengi tangu kuanza kwa msimu huu ambako nyota wake kadhaa bado wako bechi kwa majeruhi.