Chelsea,Arsenal na Mancity kucheza leo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero

Wachezaji wawili wa kilabu ya Newcastle Moussa Sissoko na Jack Colback wote watashiriki katika mechi ya leo dhidi ya Chelsea baada kusimamishwa kwa mechi kadhaa.

Favriccio Coloccini hatahivyo huenda asicheze kutokana na jeraha analoendelea kuliuguza huku Mike Wiliamson ,Daryl Janmaat na Sammy Ameobi wakiwa hawajulikani kucheza kutokanana majeraha.

Mshambuliaji ya Chelsea Diego Coast atacheza baada ya kusimamishwa kwa mechi moja huku mlinzi Gary Cahil akitarajiwa kucheza baada ya kupona jeraha.

Katika mechi kati ya Liverpool dhidi ya Sunderland,mkufunzi Brendan Rodgers lazima aamue iwapo atampumzisha Steve Gerrard kbala ya mechi ya kuwania ubingwa wa Yuropa siku ya Jumanne ambayo nisharti Liverpool ishinde ili iweze kufuzu kwa raundi ya muondoano.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mshambuliaji Alexi Sanchez wa Arsenal

Phillip Coutino amepona na Jose Enrique anatarajiwa kuanza kucheza baada ya jereha la mguu la muda mrefu.

Adam Johnson wa Sunderland na Wes Brown wanatarajiwa kurudi uwanjani kufuatia majeraha madogo.

Katika mchuano baina ya Arsenal la Stoke,wachezaji kadhaa wa Stoke wanakabiliwa na majeraha ikiwemo Glenn Whelan na Robert Huth wenye majeraha ya paja.

Vilevile Steve Sidwell,Peter Odemwinge,Victor Moses na Dionatan Texeira wote wana majeraha.

Upande wa Arsenal Nacho Monreal ana jeraha la kifundo cha mguu,huku Kierran Gibs akitarajiwa kucheza mahala pake baada ya kupata jereha la kiuno.

Haki miliki ya picha getty
Image caption Didier Drogba wa Chelsea

Wojciech Szeczesny amepoa jeraha kama hilo na sasa anatarajiwa kurudi katika goli

Koscielny na Yaya Sanogo watajaribiwa ili kuona iwapo wako tayari kucheza.

Katika mechi kati ya Manchester City na Everton,mlinzi wa Manchester City Eliakim Mangala atashiriki baada ya kusimamishwa kwa mechi moja katikati ya wili iliopita.

Aleksander Kolarov na Edin Dzeko wanaweza kurudi baada ya kuuguza jeraha la paja huku Steven Jovetic akipumzishwa.

Upande wa Everton mlinzi Antolin Alcaraz anarudi uwanjani baada ya kukosa mechi sita kutokana na jereha la bega.