Mourinho awalaumu 'ball boys' kwa kipigo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha Chelsea Jose Mourinho

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amelalama kuhusu upotezaji wa wakati baada ya timu yake kufungwa kwa mara ya kwanza katika msimu huu ugani Newcastle.

Mabao mawili ya Papis Cisse yaliiweka Newcastle kifua Mbele lakini baadaye mshambuliaji Didier Drogba akifungia Chelsea lakini bao hilo halikutosha.

''Kuna mambo ambayo yalikuwa yakifanyika bila refa kuona.Hawezi kumwaadhibu kijana wa kubeba mpira ambaye alitoweka ghafla,ama mashabiki ambao wakipata mpira wanakaa nao ama hata kuutupa uwanjani wakati mechi inaendelea''.,alisema Mourinho.

Kilabu ya Newcastle iliona mlinzi wake Steven Taylor akionyeshwa kadi nyekundu wakati ambao Newcastle ilikuwa juu kwa mabao 2-0 lakini wakaendelea na kuvunja rekodi ya Chelsea ya kutofungwa msimu huu.