Tanzania:Idris mshindi Bigbrother 2014

Image caption Mshiriki wa Bigbrother mwaka 2014

Idris Sultan mshiriki wa mashindano ya Big Brother ‘hotshots’.Toka Tanzania ameibuka kidedea wa mashindano hayo yaliyokua yakifanyika nchi Afrika Kusini.

Idris amekua Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo ,baada ya Richard Dyle Bezuidenhout; kuibuka shujaa mwaka 2011 katika Big Brother II.

Mshindi huyu anajinyakulia donge nono la Dola za marekani laki tatu,kwa kuibuka mshindi.

Tayo Faniran toka Nigeria amekuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo .

Idris alitabiriwa na wapenzi wa kipindi cha Bigbrother kuwa angeweza kuibuka mshindi kutokana na wadau wengi kuvutiwa na namna alivyokuwa akiishi katika jumba hilo la big brother pia uhusiano wake na washiriki wenzake.