Hekaheka za usajili Ulaya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jay Rodriguez ni miongoni mwa wachezaji wanaonyemelewa na Tottenham

Tottenham wanafanya mipango ya kuwapata kiungo Morgan Schneiderlin,25 pamoja na mshambuliaji Jay Rodriguez, 25,wote toka klabu ya Southampton na beki wa Raul Albiol, 29,wa Napol ya Itali ili kuimarisha kikosi chao.

Leicester City wamekata ofa ya £7.9milioni kuweza kumuuza mshambuliaji wao Andrej Kramaric, the 23 raia wa Croatia anawaniwa na timu za Chelsea na Tottenham.

Kocha wa Sunderland Gus Poyet bado anamuhitaji mshambuliaji Fabio Borini, 23, aliekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool.

Bosi wa Newcastle Alan Pardew anataka kumsajili kwa mkopo kipa Mark Schwarzer, kutoka chelsea ambae ni chaguo la tatu kwa kocha Jose mourinho.

Harry Redknapp kocha wa QPR ana imani atamsajili kwa mkopo mshambuliaji Robbie Keane, 34, nyota wa zamani wa Tottenham anayechezea timu ya LA Galaxy ya Marekani.