Man U yakwea nafasi ya tatu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Robin Van Persie wa Man U akifurahi na mchezaji mwanzake Ashley Young baada ya kufunga goli.

Manchester United al maarufu mashetani wekundu jana ilikwea hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuwaadhibu wapinzani wao Southampton kwa jumla ya magoli 2 - 1 katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa St. Marys

Kinara wa Manchester United hapo jana alikuwa ni Robin Van Persie ambaye ndiye aliyefunga magoli yote mawili kwa upande manchester United.

Kwa matokeo hayo sasa Manchester inapanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo na kuwashusha Southampton hadi nafasi ya tano.

Msimamo ulivyo kwa sasa Chelsea wapo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo, Manchester City ya Pili na Manchester United wapo nafasi ya tatu.