Kriket: Tanzania hoi kwa Kenya

Haki miliki ya picha focus bangla
Image caption Mchezo wa kriketi hupendwa sana nchini India

Michuano ya kimataifa ya mchezo wa kriketi kwa wanawake chini ya miaka 19,imeendelea kutimua vumbi mjini Dar es Salaam ambapo wenyeji Tanzania wameshindwa kutamba mbele vijana wenzao wa Kenya.

Jumla ya michezo 12 ilipigwa katika viwanja Gymkana na Anadil jijini Dar es Salaam ambapo katika mechi hiyo ya Tanzania na Kenya, Tanzania ilikubali kupokea kichapo kwa kufungwa kwa mikimbio 54 kwa 49.

Mmoja wa wachezaji wa Tanzania Winfrida Kevin anaeleza masikitiko yake baada ya timu yao kufungwa ambaye alisema kwamba walifungwa kutokana na uoga.