Arsenal yatinga 16 bora

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezaji wa Arsenal Ramsey

Club ya Arsenal imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili ya kundi D ,Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga hatua ya kumi na sita bora ya michuano hiyo ,kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Galatasaray wa nchini Uturuki.

Lukas Podolski aliifungia the Gunners bao la kwanza katika dakika ya tatu ,kabla ya Aaron Ramsey kufunga bao la pili katika dakika ya 11 na la tatu katika dakika ya 29.

Kiungo mkongwe wa Uholanzi Wesley Sneider aliifungia Galatasaray bao la kufutia machozi kwa shuti la mpira wa adhabu katika dakika ya 87 ,kabla ya Podolski kufunga goli la nne kwa Arsenal katika dakika ya 90 .

Mechi nyingine ya kundi hilo ni Borussia Dotmund imetoka sare ya bao moja kwa moja na timu ya Anderlecht ya Ubelgiji .