Kombe , Mataifa Afrika:Mali ina matumani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Mali, Sambou Yatabare

Kiungo wa Timu ya taifa ya Mali Sambou Yatabare anaamini kuwa nchi yake inaweza kunyakua Kombe la Mataifa Afrika.

The Eagles haikuwahi kushinda michuano hiyo lakini walifuzu kuingia fainali mwaka 1972, mwaka 2012 na 2013 ilishika nafasi ya tatu.

Yatabare ameiambia BBC kuwa wanajiamini kuwa wakicheza kwa nguvu zote wanaweza kushinda.

Mali ilichapwa 3-2 na Congo kwenye hatua ya fainali, miaka 42 iliyopita na kizazi hiki kina matarajio kunyakua ubingwa nchini Guinea ya Ikweta.

The Eagles ina wachezaji wenye uzoefu, kama mchezaji Seydou Keita 34, ambaye atacheza michuano yake ya saba na wachezaji wadogo wenye vipaji.

Ingawa Mali imepangwa kundi moja na Cameroon, Ivory Coast na Guinea, Eagles inaamini itafika mbali.

Yatabare ambaye alikataa kuiwakilisha nchi yake aliyozaliwa , Ufaransa, ameonekana mara 14 akiwa na timu yake ya Mali na amefunga goli moja.