Arsenal,Mancity na Chelsea uwanjani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mshambuliaji wa Mancity Kun Aguero

Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey hatacheza katika mechi dhidi ya Newcastle hii leo swala lililomlazimu kocha Arsena Wenger kumuita Francis Coquelin ambaye anaichezea kilabu ya Charlton kwa mkopo ili kuchukua mahala pake.

Walinzi Laurent Koscielny na nacho Monreal wana majeraha huku Calum Chambers akikabiliwa na marufuku ya mechi moja.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Mshambiliaji wa Chelsea Diego Costa

Newcastle watacheza bila Moussa Sissoko na mlinzi Steven Taylor ambao wamepewa marufuku ya mda.

Nahodha wao Frabricio Coloccini anatarajiwa kucheza leo huku kiungo wa kati Mehdi Abeid akitarajiwa kurudi baada ya kupata jeraha la kidole.

Viongozi wa ligi ya EPL Chelsea wana kibarua dhidi ya Hull City katika uwanja wa nyumbani wa daraja la Stamford ambapo Chelsea itajibwaga katika uwanja huo bila mlinda lango Thibaut Curtois huku Petr Cech akitarajiwa kuchukua mahala pake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mshambuliaji wa Arsena Alexi Sanchez

Cesc Fabregas ana marufuku ya mda lakini Nemanja Matic yuko tayari kuchukua mahala pake baada ya kuhudumia marufuku ya mda na hivyobasi kukosa mechi dhidi ya Newcastle ambapo Chelsea ilipoteza kwa mara ya kwanza tangu ligi hiyo ianze.

Kwa upande mwengine mlinda lango wa timu ya Leicester Ben Hamer ataanza kwa mara ya pili katika msimu huu wa EPL katika mahala pa Kasper Schmeichel ambaye anauguza jereha.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Kipa wa Chelsea apata jaraha

Nahodha wa kilabu ya Manchester City Vincent Kompany anatarajiwa kucheza katika mechi hiyo na Leicester baada ya kukosa mechi tatu kutokana na jeraha.

Kiungo wa kati David Silva na Stevan Jovetic wataorodheshwa baada ya kupata majeraha dhidi ya Roma katika mechi iliochezwa katikati ya wiki.