Man United kutoana jasho na Liverpool

Image caption Manahodha wa timu za Manchester United wayne Rooney na mwenzake wa Liverpool Steven Gerrard.timu hizo mbili zinatoana jesho leo,.

Jonny Evans huenda akaanzishwa upande wa Manchester United ili kuchukua mahala pa Chris Smalling anayeuguza Jeraha baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Southampton jumatatu iliopita.

Phill Jones na Rafael watarudi katika kikosi cha Manchester United baada ya kukaa nje kwa miezi miwili huku Angel di Maria,Luke Shaw na Dely Blind wakisalia na majeraha.

Upande wa Liverpool Adam Lallana atashiriki baada ya kupona majeraha katika mbavu zake mbili huku Kolo Toure aliyekuwa na jeraha la paja akitarajiwa kucheza.

Mario balotelli amerudi katika mazoezi na huenda akashiriki baada ya kukosa mechi sita na jeraha la paja.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Liverpool na wale wa Manchester utd katika mechi ya zamani.

Liverpool iko alama saba nyuma ya Manchester United na nyuma zaidi ya timu ilioshinda kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Old Trafford mnamo mwezi machi.

Timu hiyo imeshindwa kupata matokeo mazuri katika msimu huu huku wakiwa wamecheza mechi tano bila kufungwa kufikia sasa.

Ushindi wa Manchester United katika uwanja wa Southampton siku ya jumatatu huenda ukamfanya kocha wa timu hiyo Van Gaal kuona kana kwamba ana bahati.

Ijapokuwa rekodi yake inaonyesha kwamba kocha huyo ni mzuri,Ushindi huo uliwawacha wengi wakijiuliza iwapo timu ya Manchester United imeimarika ama bado inajikokota.