Lewis Hamilton kinara tuzo za BBC

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Nguli wa mbio za magari Lewis Hamilton

Lewis Hamiliton dereva wa timu ya Mercedes, mwenye miaka 29 ameibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya BBC ya mwanamichezo bora.

Hamilton amekua dereva wa kwanza F1 kutwaa tuzo hiyo toka alipofanya hivyo Damon Hill ,mwaka1996.

Akielezea furaha yake Hamilton alisema"Asante kwa mashabiki wote huwa nasema tunashinda na kupoteza pamoja nahisi upendo wenu itaendelea kufanya muwe na fahari. "

Nyota huyo wa mbio za magari alipata kura 209,920 na kufanikiwa kuwashinda mcheza gofu namba moja dunia Rory Mcllroy na Mwanariadha Jo Pavey.