Kobe Bryant amzidi Jordan NBA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nguli wa vikapu Kobe Bryant

Mchezaji mashuhuri wa timu ya Los Angeles Lakers kobe Bryant amefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwa ufungaji wa muda wote katika ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani(NBA)

Kobe mwenye miaka 36, amefanikiwa kuvuka idadi ya pointi alizofunga nyota wa zamani wa mchezo huo Michael Jordan.

Nyota huyu wa kikapu alifanikiwa kufunga pointi 26 katika mchezo uliopita na kufikisha pointi 32,310 katika michezo1,269 na kumzidi Jordan mwenye pointi 32,292 katika michezo 1,072 aliyocheza.

"Nimekwenda kwa kasi kweli na ni hatua kubwa, najaribu kujifunza zaidi kutoka kwake(Jordan)amekua sehemu ya mafanikio yangu kwa kunipa ushauriā€¯.alieleza Kobe Bryant.

Kareem Abdul Jabbar ndio anaongoza kwa kuwa mfungaji wa muda wate kwa kuwa na jumla ya pointi38 387 akifuatiwa na Karl Malone mwenye pointi 36 928.