Steve smith:nahodha mpya wa australia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Steven Smith

Steve Smith, ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Australia, ya mchezo kriketi akichukua mikoba ya Michael Clarke.

Smith mwenye miaka 25,anakua nahodha wa 45 kukiongoza kikosi cha kriketi cha Austalia na wa tatu kwa udogo kuwahi kuwa nahodha.

Brad Haddin ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa wa timu hiyo.

Mwenyekiti Rod Marsh, ameeleza katika taarifa : " Tunampongeza Steve ni heshima ya ajabu kuingoza nchi yake.”

Uchaguzi huu wa nahodha mpya umekuja baada ya aliekua nahodha wa timu hiyo Michael Clarke kupata maumivu ya mgongo