Nusu fainali ya klabu bigwa ya dunia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vijogoo barani Ulaya

Mabingwa wa Ulaya Real Madrid, wataingia dimbani kucheza na Mabingwa wa Concacaf Cruz Azul ya Mexico. Katika mchezo wa kombe la klabu bigwa ya dunia Usiku wa jumanne huko Mjini Marrakech Nchini Morocco.Nusu Fainali nyingine itachezwa Jumatano Usiku kati ya San Lorenzo ya Argentina na Auckland City ya New Zealand.

Wakati Real wanaanza hatua ya Nusu Fainali, Cruz Azul walianzia Robo Fainali na kuibwaga Western Sydney Wanderers ya Australia kwa Bao 3-1 katika Mechi iliyopigwa Dakika 120 baada ya kwenda sare ya goli 1-1 katika Dakika 90 za mchezo.

Real watakuwa wakisaka Taji lao la 4 kwa Mwaka 2014 kitu ambacho hawajahi kufanya baada ya kuwahi kutwaa Mataji Matatu ndani ya Mwaka mmoja.

Real Madrid watawakosa Mastaa wao James Rodriguez na Luka Modric ambao ni majeruhi huku Sami Khedira pekee akiwa na uwezekano wa kucheza Fainali ikiwa watafuzu kuitoa Cruz Azul.